Wakazi "Mziki wa Singeli Unachukua Nafasi ya Mziki wa Hip Hop Tanzania"


Huu Hapa Ujumbe Wa Rapper @wakazi Baada Ya Kupost Ngoma Mpya Ya dullamakabila .......''THIS IS NICE @dullamakabila 🔥🔥

Maudhui ✅
Ubunifu wa wimbo ✅
Ubunifu wa video ✅

Sound ya Singeli ni unorthodox, ikimaanisha ni ya kipekee na kitofauti, hivyo inaeleweka kama kuna watu hawatoipenda au ku-relate nayo. Ila mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni. Singeli imepiga hatua kubwa na inafurahisha kuona umekuwa ni commercial mainstream music sasa (social platform trending) 👏🏾

Wiki kadhaa zilizopita nilizungumza kwenye kongamano la ACCES (clip ipo inazunguka shot by wasafi media) na nilisema kuwa nina amini kuwa Singeli imechukua au inaenda kuchukua nafasi ya Hip Hop, kama muziki wa uhalisia wa maisha ya kila siku, na wenye maudhui ya kufikirisha. YAANI KIUFUPI THEY KEEP IT REAL. Meja Kunta, Sholo Mwamba,Kinata Mc na hadi Dula Makabila (na wana kibao tu wengine), wanaibeba bendera vizuri. Na it is a nice thing kuona inapokelewa kwa ukubwa. HONGER DULLA, KAZI NZURI

ILA HONGERA KWA WOTE WANAOIFANYA, INUA NA KUIPIGANIA SINGELI.

The Leader.''

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad