Wakicheza Bila Kiungo wao Fei Toto Timu ya Yanga imeichapa Azam FC Kibabe


WAKICHEZA bila kiungo wao Fei Toto timu ya Yanga imeichapa Azam FC mabao 3-2 mchezo wa Ligi Kuu ya NBCD uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar Es Salaam.


Azam FC walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Abdul Sopu dakika ya 27 akimalizia pasi ya Prince Dube huku Yanga wakipata mabao kupitia kwa Fiston Mayele dakika ya 31 na Stephane Aziz Ki dakika ya 33 na kuenda mapumziko Yanga wakiwa wanaongoza.


Kipindi cha pili Azam FC walipata bao la mapema dakika ya 47 likifungwa na Abdul Sopu na bao la ushindi la Yanga likifungwa na Farid Mussa dakika ya 78.


Kwa ushindi huo Yanga wamefikisha Pointi 47 na kuiacha Azam FC kwa tofauti ya Pointi 10 huku wakicheza bila kiungo wao Fei Toto anayedaiwa kusajiliwa na Azam FC.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad