Mahakama kuu Kanda ya Dar es salaam imewahukumu watuhumiwa 11 wa kesi ya mauaji ya mwanaharakati mpinga ujangili wa tembo, Wayne Lotter aliyeuawa Masaki jijini Dar es Salaam wamehukumiwa kunyongwa Hadi kufa baada ya mahakama kuwakuta na hatia ya kosa la mauaji.
Hukumu hii imesomwa na Jaji Leila Mgonye wa mahakama kuu ya Tanzania baada ya kujiridhisha na ushahidi wa upande wa mashtaka kupitia mashahidi wake 32 unaowatia hatiani
bila kuacha mashaka yoyote.
Baada ya kumaliza kusoma hukumu hiyo, iliyosomwa kwa zaidi ya masaa matano, Jaji Mgonye amebainisha kuwa watuhumiwa hao wanaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo kama hawajaridhiahwa na maamuzi hayo dhidi yao.
Waliotiwa hatiani na kuhukumiwa adhabu hiyo ni Rahma Almas, mkazi wa Mbagala B, Nduimana
Ogiste, maarufu kama mchungaji na raia wa Burundi,
Godfrey Salamba mkazi wa Kinondoni Msisiri A na
Chambie Juma Ally, mkazi wa Kia/Boma.
Wengine ni ni Allan Elikana Mafue; Ismail Issa Mohammed
(Machipsi), Leornad Phillipo Makoi, Ayoub Selemani
Kiholi; Abu Omary Mkingie na Habonimanda Augustine
Nyandwi (pia raia wa Burundi) na Michael Dauv Kwavava.
Wayne ambaye alikuwa mwanzilishi wa PAMS Foundation, taasisi ambayo ilikuwa mstari wa mbele kusaidia kupambana na uwindaji haramu na biashara ya pembe za ndovu nchini Tanzania aliuawa Agosti 16, 2017 wakati akitoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere akielekea nyumbani kwake Masaki.
Baada ya hukumu hiyo Watu waliohukiwa ambao ni wanaume 10 na mwanamke mmoja, ambao wanaume hao 10 wamepelekwa Gereza la Ukonga na Mwanamke akipelekwa Gereza za Segerea