Mapya yaibuka !! Wanasayansi wameanza kufikiria kutengeneza tumbo feki la uzazi ili kuweza kuwa na kiwanda cha kukuza watoto ambapo kwa mwaka uvumbuzi huo unaweza kutoa watoto 30,000 maabara au katika kiwanda kimoja
Wazo hilo limetolewa na influencer wa kisayansi kutoka nchini Yemen, Hashem Al-Gaili ambaye pia ameachia mfano wa video ya tumbo feki la uzazi ambapo video imeonesha matumbo feki ya uzazi yakiwa yamejazana kiwandani
Amesema hilo bado ni wazo na ikiwa litafanyiwa kazi basi litasaidia wanawake wengi ambao kwasasa hawawezi kubeba mimba wao wenyewe kwasababu mbalimbali yakiwemo magonjwa yanayopelekea waondolewe tumbo la uzazi
Pia amesema huduma hiyo ya kukuza watoto kiwandani kupitia tumbo la uzazi la uongo itasaidia sana nchi ambazo kwasasa zimekumbwa na uhaba mkubwa wa watoto kuzaliwa hivyo idadi ya watu kupungua katika nchi hizo zikiwemo Bulgaria, Japan na Korea Ya Kusini
Katika huduma hiyo ya tumbo feki kukuza watoto kiwandani, mzazi atakuwa na uwezo wa kuchagua muonekano wa mtoto ikiwemo rangi ya ngozi, nywele, macho, kimo na yote yanayohusu genetic na hata kuepuka magonjwa ya kurithi, pia kuchagua uwezo wa kiakili
Katika huduma hiyo kiwandani mtoto atazaliwa kwa kubonyeza tu kitufe flani kisha anatoka tofauti na inavyokuwa kwa mama
Wazo hilo la kisayasi na video ya mfano toka kwa influencer husika wa Yemen limesambaa ghafla ikiwemo katika vyombo vingi vya habari mataifa ya Ulaya, America na Asia
Ikumbukwe kupandikiza mtoto maabara miaka ya mwanzo lilikuwa kama wazo tu baadaye likawa rasmi baada ya wanasayansi kulifanyia kazi na kwasasa imekuwa kama kawaida watu kupata watoto kwa njia ya upandikizaji hasa nchi za nje ya Africa