Wanasayansi wa Ufaransa wamefufua na kugundua "virusi vya zombie" vya umri wa miaka 48,500 vilivyozikwa chini ya ziwa lililoganda huko nchini Urusi.
Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali kutoka kwenye mitandao mkubwa duniani, zinaeleza kuwa sampuli hizo zilikusanywa kutoka katika eneo la Siberia nchin Urusi, na kufufua vimelea vipya 13 "vilivyohifadhiwa chini ya ziwa kwa zaidi ya miaka 48,500 iliyopita." Na Waligundua kuwa virusi hivi hubakia kuambukiza licha ya kuwa wamelala kwa mamia ya milenia.