Watu 14 Wakamatwa Baada ya Kudanganya Kuna Mama Mjamzito Anataka Kujifungua Kwenye Ndege



Polisi wa Uhispania wamewatia mbaroni abiria 14 akiwemo mama mjamzito baada ya kusababisha ndege ya kibiashara kutua kwa dharura ikiripotiwa mama huyo alikuwa akitaka kujifungua.

Ndege hiyo ilikuwa ikitoka Morocco kuelekea Uturuki ililazimika kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa El Prat eneo la Barcelona mapema Jumatano baada abiria kudai kuwa mama mjamzito alikuwa amefikia muda wa kujifungua.

Inaripotiwa kuwa wakati ndege hiyo ilipotua ilikuwa imesubiriwa na ambulensi na askari waliokuwa wamepiga doria kwenye uwanja wa ndege na ilipotua abiria 28 kati ya 228 waliokuwa kwenye ndege hiyo wakuwa wanajaribu kutoroka.

Polisi walifanikiwa kuwashikilia 14 kati yao, akiwemo mwanamke huyo mjamzito. Wengine 14 walitoroka baada ya ndege kutua.

Mwanamke huyo mjamzito alichunguzwa hospitalini na kugundulika kuwa hana maumivu ya kujifungua, polisi walisema.

Hilo sio tukio la kwanza kutokea kwai mnamo Oktoba mwaka jana, kundi la abiria lilifanya njama ya kutaka ndege kutua kwa dharura kwenye kisiwa cha Mallorca nchii Uhispania kufuatia dharura za uongo.

Abilia 12 kati yao walikamatwa huku wengine 12 wakitoroka.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad