Waziriri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dr. Dorothy Gwajima amesema kuna haja ya kufunga camera kwenye Mabasi yanayowabeba Wanafunzi (School Bus) ili kudhibiti vitendo vya ubakaji na ulawiti kwa Watoto vinavyofanywa na baadhi ya Madereva na Makondakta huku pia akisema School Bus zote badala ya kuwa na Wanaume wawili (Dereva na Kondakta), lazima mmoja awe Mwamamke.
Waziri Gwajima ametoa ushauri huo baada ya sakata la Dereva na Kondakta wa Basi la Shule ya Starlight Pre and Primary kushikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumbaka na kumlawiti Mwanafunzi wa Kike wa Shule hiyo mwenye umri wa miaka sita.
Gwajima amesema “Watuhumiwa wako ndani na wameshapanda Mahakamani (pongezi wote waliowajibika haraka), kesi inaendelea”
“Hakuna namna inabidi School Bus zote badala ya kuwa na Wanaume wawili mmoja Dereva na mwingine Konda, lazima mmoja awe Mwanamke na hapa hakuna cha gharama kuongezeka mana ni Jinsia tu ndiyo inabadilika, hii itawezesha ulinzi imara wa Mtoto wa kwanza kuchukuliwa na wa mwisho kurejeshwa, tunaungana na tamko la DC wa Kinondoni, Godwin Gondwe”
“Huko mbele kuna haja ya kufunga na camera kwenye hizi School Bus, tunaangalia uwezekano, lazima Wateja walindwe yaani Mtoto ni mteja jamani inakuwaje analipia huduma halafu anakatiliwa ???”