Klabu ya Azam FC kupitia kwa msemaji wake Hashim Ibwe imethibitisha kuwa Yanga SC imebisha hodi klabuni hapo kwa ajili ya saini ya wachezaji wake wawili mshambuliaji Kipre Junior na kiungo James Akaminko.
"Azam FC inathibitisha kupokea maombi ya Yanga sc mapema leo juu ya uwezekano wa kunasa saini ya nyota wetu wawili James Akaminko na Kipre Jr. Maombi yamepokelewa na hivi karibuni watajibiwa kama wanapatikana au la!" Ameandika @hasheem_ibwe kupitia ukurasa wake Twitter.