Yanga Yafanga Kweli, Mayele Hakuna wa Kumzuia Bongo


IMEKUWA ni kawaida kwa straika wa Yanga, Fiston Mayele kutupia kila anapokutana na Coastal Union ya Tanga, katika mchezo wa leo ndiye aliyeanza kucheka na nyavu dakika 29, akipokea pasi ya Joyce Lomalisa na 47 asisti ya Aziz Ki.

Kuanzia dakika ya kwanza hadi 32 wachezaji Coastal Union walikuwa wanakaba mtu na mtu, baada ya bao hilo walianza kurudi nyuma huku kipindi cha pili Yanga ilirejea kwa kasi.

Yanga katika mchezo huo imeibuka na ushindi wa mabao 3-0, Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku Coastal Union ikifungwa mechi mbili mfululizo, ilianza kupoteza na KMC kwa bao 1-0, mchezo uliopigwa Desemba 15, Uwanja wa Uhuru.

Bao la tatu la Yanga lilifungwa na Feisal Salum 'Fei Toto' dakika ya 66, akipokea pasi ya Aziz Ki na kufikisha la sita kwenye chati ya ufunga kwenye ligi.

Ukiachana na Yanga kupata ushindi huo, straika wao Mayele anakuwa kinara kwa mabao 13, akibakiza matatu kufikia 16 aliyomaliza nayo msimu uliopita nyuma ya George Mpole (17) wakati yupo Geita Gold.
Katika mechi 17 Yanga imeshinda 14, sare mbili, kapoteza mmoja dhidi ya Ihefu, inamiliki pointi 44, wakati Coastal Union kwenye mechi 17 imeshinda nne, sare tatu, imepigwa 10 ina pointi 15 na ipo nafasi 13 katika msimamo.

REKODI ZA MISIMU YA HIVI KARIBUNI
2020/21
Yanga 3-0 Coastal Union, ilikuwa Oktoba 3,2020.
Coastal 2-1 Yanga, Machi 4, 2021.

2021/22
Coastal Union 0-2 Yanga, Januari 16, 2022
Yanga 3-0 Coastal Union, Juni 15, 2022.
2022/23
Coastal Union 0-2 Yanga, Agosti 20, 2022
Yanga 3-0 Coastal Union, Desemba 20, 2022.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad