Afande Sele Apinga Ujio wa Kocha Robertinho Simba " Yanga na Simba ni Kaburi la Soka Bongo"



Msanii Mkongwe na Gwiji wa Muziki wa Kizazi kipya Seleman Msindi ‘Afande Sele’ amezibwatukia Klabu za Simba SC na Young Africans kwa kuzitaja kama makaburi ya Soka la Bongo.


Afande Sele ambaye si mara kwa mara zote husikika akizunguza Soka la Bongo, lakini anapotoa kauli ama andiko basi huwa na mguso kwa wahusika na kuzua mjadala mzito katika jamii ya mchezo huo.


Gwiji huyo ametoa andiko lake akizilaumu Simba SC na Young Africans kwa kusema zimekua zikiuwa Soka la Tanzania na akaenda mbali zadi kwa kutoa shutuma za kupanga matokeo kwa kununua wachezaji wa timu pinzani na waamuzi, ili kushinda michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, eti kwa kizingizio cha Kuwa Mabingwa.


Mkongwe huyo pia amegusia suala la Simba SC kumleta Kocha Mkuu mpya kutoka nchini Brazil Roberto Oliveira Gonçalves do Carmo ‘Robertinho’, ili hali tayari wamekua na Kocha Mzawa Juma Ramadhana Mgunda, ambaye ameonesha kuwa na mustakabali mzuri wa kuipa matokeo timu katika Michuano ya Kimataifa na ile ya ndani ya Tanzania Bara.


PICHA: Mwamba amerudi Paris-Ufaransa

Andiko la Afande Sele linasomeka hivi: Hata sijui ni kipele gani huwa kinawawasha viongozi wa timu zetu hizi zilizozeeka bila kuwa na historia za maana kwenye mpira wa Africa zaidi ya kubadilishana ubingwa wa ndani ya nchi zenyewe miaka yote huku sababu kuu ya ubingwa wao ukiwa ni kununua mechi kuanzia kwa wachezaji wa timu pinzani hadi waamuzi.🤬


Tukiachana na ushabiki maandazi wa kikondoo utagundua kuwa Simba na Yanga ndio kama makaburi ya mpira wa Bongo kutokana na aina ya viongozi wake wazugaji na wapigaji na pia kutumika kisiasa nje ya kanuni sahihi za mpira👣


Hizi timu zee ndio zinaongoza kutumia pesa nyingi kila msimu kwajili ya usajili wa wachezaji wa nje na ndani ya nchi lkn pia ndio timu zinazoongoza kununua hata mechi na timu ndogo ili kupanga matokeo ndani ya uwanja👌


Hayo yote yanasababishwa na kuongozwa na waganga njaa au watu wanaotafuta maslahi yao ya kisiasa lkn hawana maarifa yoyote kuhusu mpira wa miguu.⚽


Nelson Okwa: Sijui lolote kuondoka Simba SC

Kwa mfano Simba ya msimu huu na msimu uliopita tangu mwanzo tuliona kuwa usajili wake sio mzuri kivile kama hadhi na ukubwa wa timu..na hii ni kwasababu mdhamini Mo ni kama alishaanza kuikataa timu kiana na sisi wengine tuliona hilo mapema ingawa tuliposema ukweli huo makolo wenzetu wakatujia juu na kuongea kila aina ya kashfa sawa na wakati ule nilipowaonya makolo wenzangu kuhusu “usnitch” wa Manara enzi zile akiwa Simba hadi walipoyaona kwa macho yao wenyewe👀


Wote tunajua kama Simba ya wakati huu inashida nyingi za kiuchumi kwakua mdhamini mkuu haeleweki yupo mguu nje mguu ndani hivyo timu inatakiwa ijibane sana kuepuka matumizi makubwa yasiyokua ya lazima kama swala la kuchukua kocha wa nje wa gharama kubwa ktk wakati ambao timu inakocha mzawa na anaefanya vyema pamoja na udhaifu wa kikosi uliosababishwa na mdhamini “Janjajanja”.😫


Chama awabwaga Bocco, Kapombe Simba SC

Sioni sababu wala ulazima wowote wa Simba kuchukua kocha wa nje wakati huu zaidi ya muendelezo uleule wa wapigaji wa timu hizi kutafuta ten pacent kwenye mikataba ya kuwanunua hata kwenye mishahara ya hao walimu na baadhi ya wachezaji vilaza kutoka nje..👉


Baada ya usanii huu wa kipuuzi waliofanya viongozi wa Simba sitoshangaa kuona timu ikivurugika na kupoteza mwelekeo zaidi badala ya kuimarika..💪


Each one Teach one.✍️

@afandesele1976

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad