Afisa wa polisi aliyemuua Mmarekani mweusi George Floyd ataka kesi yake ifutwe




Afisa wa polisi ambaye alimuua Mmarekani mwenye asili ya Afrika George Floyd na kuibua hasira kubwa nchini Marekani mwaka 2020 anajaribu kuanzia Jumatano hii ili hukumu yake ya mauaji ifutwe.

Derek Chauvin, 46, alipatikana na hatia ya mauaji na mahakama ya kaskazini mwa jimbo la Minnesota kufuatia kesi inayomkabili na ambayo iligonga vichwa vya habari mwaka 2021 na kuhukumiwa kifungo cha miaka 22 na nusu jela.

Anaamini kwamba haki zake katika kesi isioegemea zimekiukwa, hasa kutokana na "utangazaji" kuhusu kesi hiyo na "vitisho vya vurugu" ambavyo vilisababisha mabadiliko ya kimazingira wakati kesi hiyo ilipokuwa ikisikilizwa mahakamani, na kutaka uamuzi huo ufutiliwe mbali.

Licha ya maombi hayo, Derek Chauvin atasalia gerezani kwa sababu alikiri hatia ya "ukiukaji wa haki za kiraia" kwa George Floyd mbele ya jaji wa shirikisho na akapokea hukumu ya mwisho ya miaka 21 jela mnamo 2022.


Mnamo Mei 25, 2020, afisa huyu wa polisi wa Minneapolis, ambaye alikuwa akihudumu kwa miaka 19, alipiga goti juu ya shingo la Mamrekani huyo mweusi kwa karibu dakika kumi, bila kujali kelele za wapita njia waliojawa na hofu.

Tukio hilo, lililorekodiwa na kuchapishwa mtandaoni, lilizua maandamano makubwa dhidi ya ubaguzi wa rangi na ukatili wa polisi kote Marekani na kwingineko duniani.

Wakati wa kesi katika mahakama ya eneo hilo, wakili wake aliomba kwamba George Floyd alikufa kutokana na matumizi ya nguvu ya kiasi, pamoja na matatizo ya kiafya, na akahakikisha kwamba Derek Chauvin alitumia nguvu.


Leo, afisa huyo wa zamani wa polisi anatafuta kubatilisha kesi hii, haswa kwa sababu ilifanyika katika miji pacha ya Minneapolis-Saint-Paul, ambayo ilikuwa bado iko ukingoni chini ya mwaka mmoja baada ya mkasa huo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad