Aliyeuwa watu 21 atengewa dola Mil. 10




Serikali ya Marekani imetenga dola milioni 10 kwa taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwa muhusika mkuu wa shambulio la kigaidi dhidi ya hoteli moja ya nchini Kenya, Hamoud Abdi Aden aliyesababisha vifo vya watu 21 mwaka 2019.

Al Shabab, kundi lenye mafungamano na Al-Qaeda, lilidai kuhusika na shambulio hilo la Januari 15, 2019 katika hoteli ya DusitD2 iliyopo mji mkuu wa Kenya Nairobi, katika shambulio lililodumu kwa takriban saa ishirini.


Wahudumu wa Afya wakimpokea mtu mmoja katika hospitali ya Garissa baada ya kujeruhiwa katika shambulio hilo. Picha ya Stringer/ AFP.
Balozi wa Marekani nchini Kenya, Meg Whitman amewaambia waandishi wa Habari jijini Nairobi kuwa Marekani imetenga zawadi ya hadi dola milioni 10 kwa habari zitakazowezesha kukamatwa kwa mtu huyo.

Naye Mkuu wa Kurugenzi ya Uchunguzi wa Makosa ya Jinai nchini Kenya, Amin Mohamed Ibrahim, amesema kundi la Al Shabab, limemefanya mashambulizi kadhaa Kenya tangu nchi hiyo ilipotuma jeshi lake nchini Somalia mwezi Oktoba 2011, kupigana dhidi ya kundi hilo la Kiislamu lenye itikadi kali.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad