Aumuzi Mgumu Unakuja Simba, Chama Aistua


KOCHA Roberto Oliviera ‘Robertinho’ akiiongoza Simba kwa mara ya kwanza kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara, juzi Jumatano akianza na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mbeya City, lakini hatua yake ya kumtoa Clatous Chama uwanjani kipindi cha kwanza kilishtua mashabiki.

Kocha huyo alimtoa Chama na John Bocco aliyeumia dakika ya 33 na kuwaingiza Pape Ousmane Sakho na Kibu Denis na kufanya mashabiki kupigwa na butwaa na wengine kuzomea, wakati matokeo yakiwa bao 1-1.

Hata hivyo, kocha huyo alisema mara baada ya mechi hiyo kwamba kuna maamuzi magumu atafanya kikosini kwa malengo ya kujenga na kuwapa furaha mashabiki.

Katika mchezo huo uliopigwa Kwa Mkapa, Saido Ntibazonkiza aliitanguliza Simba kwa bao dakika ya 11 akimalizia pasi ya Chama kabla ya City kuchomoa dakika mbili baadaye kupitia Richard Ng’ondya..

Ndipo Bocco akaumia na Kocha Robertinho akamtoa pamoja na Chama aliyepitiliza hadi vyumbani kisha kurejea benchi, huku mashabiki wakionekana kupagawa na mabadiliko hayo wasiamini walichokiona.

City ilicheza kwa nidhamu na kujilinda, sambamba na kushambulia hasa kipindi chwa kwanza, huku Salim Kihimbwa akiisumbua ngome ya Simba.

Kipindi kipindi cha pili, Simba ilianza kwa kasi na kupata penalti dakika ya 49 baada ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kuchezewa faulo na Ng’ondya. Mwamuzi Esther Adalbert aliamuru adhabu hiyo na Saido akatupia bao la pili na la tisa kwake msimu huu akilingana na Bocco. Hilo ni bao la tano kwa Saido tangu ajiunge Simba

Sakho aliiongezea Simba bao la tatu kwa shuti kali la mbali dakika ya 56 likiwa la sita kwake msimu huu kabla ya City kupata pigo kwa Samson Madeleke kulimwa kadi kwa kumchezea vibaya Sakho dskika ya 66’

Hata hivyo, katika dakika ya 78, Juma Semvuni alimtungua kipa Aishi Manula kwa mpira mrefu alioudakia nyavuni. Ushindi huo umeifanya Simba ifikishe pointi 47 baada ya mechi 20, sita pungufu na ilizonazo Yanga (53).
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad