Binti mmoja toka nchini Bangladesh ameingia kwenye headlines za dunia baada ya kupiga mbizi toka nchini humo hadi India kwa ajili ya kwenda kumuoa Kijana mmoja ambaye alikuwa mchumba wake.
Binti huyo kwa jina Krishna Mandal (22), aliishia kukamatwa na polisi wa Narendrapur kwa kuingia nchini India kiharamu. Kwa mujibu wa taarifa, Krishna alitumia takribani saa moja akiupasua mto Matla huku mpenzi wake akiwa anamsubiri na gari kando ya mto huo. Baada ya kufika, waliendesha hadi Kijiji cha Kolkata ambapo walifunga ndoa.
Jambo gani la hatari uliwahi kulifanya kwa ajili ya mapenzi?