Inafikirisha...Kajala Anafanya Kazi Gani?


Kajala haigizi Filamu, Sio balozi wa kampuni yoyote. Je, anapata wapi hela za kula bata, kwenda South, kununua Crown ya Paula?

Kajala angekuwa na Biashara lazima tungejua tu Maana ange-post ili apate wateja wengi zaidi.

Kajala huwa anasema ana kampuni ya Filamu lakini sijawahi kuona hata kichekesho cha dakika moja kutoka kwenye kampuni hiyo.

Shule huko kuna watoto wanatamani kuacha Shule ili wawe kama kajala lakini Kajala amewaficha baadhi ya Vitu, hawajui anafanya kazi gani, huenda wangejua kazi anazofanya ili aishi wangeacha kabisa kutamani kuwa kama yeye.

Ukiona mtu Maarufu anaishi vizuri na kazi anayofanya haijulikani inabidi uwe makini sana.

Video Vixen, Ma-star wakike Bongo Movie na Bongo Fleva wana siri nzito sana. 
Watoto wa Shule msitamani maisha ya watu ambao hamjui kiundani wanaishi vipi, wanaingizaje pesa

By Hopetyga 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad