Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan ametangaza kuruhusu mikutano ya hadhara ya Vyama vya siasa nchini Tanzania na kuondoa marufuku iliyokuwepo kwa muda mrefu.
Rais Samia ameyasema haya mbele ya Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vya Siasa Ikulu Dar es salaam leo ambapo amenukuliwa akisema “Uwepo wangu mbele yenu leo ni kuja kutangaza kwamba lile tangazo la kuzuia mikutano ya hadhara sasa linaondoka”.
Mkutano huu wa leo umehudhuriwa na Viongozi wa Vyama vya siasa mbalimbali akiwemo Freeman Mbowe wa CHADEMA, Profesa Lipumba wa C.U.F na Zitto Kabwe wa ACT.