Rais Samia Suluhu Hassan.
Taarifa iliyotolewa leo Januari 24, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, imewataja waliotenguliwa kuwa ni Reuben Ndiza Mfune, Mkuu wa Wilaya ya Mbarali na Msongela Palela, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma mkoani Mara.
Wengine waliotenguliwa ni Michael Matomora, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Singida, Linno Mwageni, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ushetu, Shinyanga na Sunday Ndori, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Njombe.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa utenguzi huo ulianza Januari 22, 2023.