Staa wa Muziki kutoka Nchini Nigeria Burna Boy ametajwa kumpa Mwandishi wa Habari wa Ufaransa Zaidi ya Milioni 4 kwa ajili ya kwenda kurekebisha Camera yake ambayo aliiangusha wakati akimkimbilia kufanya nae mahojiano.
Mwandishi wa Habari huyo ambae anatajwa kuwa katika mafunzo kwa bahati mbaya aliangusha Camera yake wakati alipokuwa akikimbia kwenda kumfanyia mahojiano Staa huyo.
Kwa mujibu wa Vyombo vya Habari vya Ufaransa, Camera hiyo ilikuwa ni aina ya Panasonic GH6 yenye thamani ya dola za kimarekani Laki mbili($2000).
Burna Boy inasemekana aliona tukio hilo na kumuagiza muhasibu wake kumpa Mwandishi kiasi hiko cha fedha kwa ajili ya matengenezo ya Camera hiyo.