Msanii wa filamu ambaye kwa hivi sasa anafanya vizuri sana kupitia filamu za Kibongo na video vixen, Careen Simba @caren_simba amesema anawachukia wanaume ambao hawawapi fedha wapenzi wao wala hawawajali na kuwahudumia.
Ameongeza kuwa jukumu la mwanaume siku zote ni kumpa fedha mpenzi wake na anavyompa si kama anamhonga bali ni kumlinda na kumhudumia.
“Hakuna kitu ninachochukia kama mwanaume kuona kuwa kumpa pesa mwanamke ni kumhonga wakati ni jukumu lake.
"Kama ni mwanamke wako lazima umhudumie ingawa na yeye anatakiwa afanye kazi, siyo kila kitu mpaka amwambie mwanaume wake," amesema.
Amesema kuwa siku zote anaamini kuwa mwanamke kama utajitambua mwenyewe na kujiheshimu hakuna mwanaume au mtu yeyote anayeweza kukusumbua.
Careen ambaye pia ni baby mama wa msanii wa Bongo fleva, Barakah The Prince,amesema hakuna kitu anachokithamini na kuona anajukumu nalo kama kumuangalia mtoto wake kipenzi na kuhakikisha anapata anachostahili.
" Siku zote mwanamke mwenyewe ndio wa kujiweka kwenye nafasi unayotaka na sio mtu mwingine,hivyo ukichagua kujithamini na kujiheshimu na wengine watafanya hivyo, na kwa upande mtoto wangu ndio jukumu langu la kwanza" alisema Careen
Kwa sasa mrembo huyo anafanya vizuri sana kwenye filamu na ndio msanii ambaye ana mkwanja mrefu kwa sasa.
Pia msanii huyo aliongeza kuwa ni wajibu kila msanii kutambua nyakati zilizopo,kwa maana kuna wakati hata nafasi yako ya kuigiza inaweza kufika mwisho na ukawa hauna ulichokipanda kwa kipindi chote.
" Wasanii tusijisahau sana kwa kipindi hiki ambacho tunacho kwasababu kuna muda unafika wataibuka watu wengine kabisa na sisi tutasahaulika hivyo ni vyema kujitengenezea mazingira mapema kabisa"alisema Careen