KOCHA wa zamani wa Sports Club Villa ya Uganda, Edward Kaziba amewaonya wachezaji wa Simba wakiwemo viungo wa ushambuliaji Mzambia, Clatous Chama na Saidi Ntibanzokiza ‘Saido’ raia wa Burundi kuwa kama wanataka kufanya vizuri wakiwa chini ya kocha mpya Roberto Oliveira ‘Robertinho’ basi ni lazima wawe watulivu kutokana na ukali alionao kocha huyo.
Kaziba ambaye kwa sasa ni miongoni mwa makocha wa timu za taifa za wanawake nchini Uganda ametoa kauli hiyo kufuatia Simba kumtangaza Robertinho, raia wa Brazil kuwa kocha mkuu akichukua iliyokuwa ikikaimiwa na Juma Mgunda ambaye anaenda kuwa kocha msaidizi atakayesaidia na Seleman Matola.
Chama mwenye mabao matatu pamoja na asisti 11 huku Saido akiwa na mabao saba kwenye ligi kutokana na kuweka rekodi ya kufunga hat trick katika mechi yake ya kwanza msimu huu tangu ajiunge na Simba kwenye usajili wa dirisha dogo.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Kaziba alisema kuwa moja ya sababu iliyopelekea kwa Mbrazil huyo kufanikiwa kwenye soka la Uganda na Afrika Mashariki ni kitendo chake cha kusimamia nidhamu kwa ukubwa hivyo wachezaji wa Simba wanatakiwa kuwa makini ikiwa wanataka kuendelea kufanya vizuri msimu huu chini ya kocha huyo.
“Binafsi ni mjua kwa sababu alikuwa hapa Uganda na Vipers ambayo ukweli kazi yake kila mmoja ameiona na siku kushangaa kusikia ameenda Simba maana Simnba ni mmoja kati klabu kubwa hapa Afrika Mashariki na Kati na imekuwa ikifanya vizuri katika michuano ya kimataifa hivyo hakuna kocha ambaye hatamani kuona anaweza kufanya nao kazi.
“Lakini kitu ambacho antaka kuwashauri wachezaji wa Simba ni kuwa makini na suala la nidhamu zao kwa sababu huyu kocha ambaye wapo naye kwa sasa siyo mtu wa mchezaji na mkali kwa mambo ambayo kwake anaona haya msingi, nadhani ndiyo kityu ambacho wachezaji wanatakiwa kuwa nacho makini kwa kuwa mtu mwenye siyo mgeni wa soka la Afrika Mashariki, amekuwepo kwa muda mrefu,” alisema Kaziba.
Stori na Ibrahim Mussa