Dawa Mpya ya Kuponesha Ukimwi Yaidhinishwa, Matumaini Yarejea


MAMLAKA inayoshughulika na uidhinishaji Dawa na Chakula nchini Marekani (FDA) imeidhinisha dawa inayoweza kutibu ugonjwa wa Ukimwi miongoni mwa watu wazima kwa kuitumia mara mbili kwa mwaka. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Wagonjwa wanapewa dawa hiyo mara mbili kwa mwaka kwa njia ya kudungwa sindani au kumeza tembe. Dawa hiyo inagharimu dola 42,250 za Marekani (sawa na Sh 99 milioni) kwa awamu hizo mbili.

Watumiaji pia wanahitajika kutoboka dola 39,000 (Sh91.1 milioni) kila mwaka kugharamia dozi za utunzaji.

Wakati huu, dawa sawa na hiyo inayojulikana kama Cabenuva (cabotegravir and rilpivirine) kutoka kampuni ya dawa ya Uingereza ya GSK, inagharimu dola 40,000 hadi dola 50,000 (Sh93.4 milioni hadi Sh117 milioni) kwa mwaka.

Mwaka 2021, dawa hiyo ambayo mgonjwa hupewa kwa kudungwa sindano, ilikuwa ya kwanza kuidhinishwa na FDA kama tiba ya ugonjwa huo unaosababishwa na virusi vya HIV.

Kulingana na wataalamu, dawa ya sasa inayojulikana kama Sunlenca (lenacapavir) inatumiwa kutibu watu ambao miili yao ni sugu kwa dawa mbalimbali.

“Uidhinishwaji huo unachangia uwepo wa aina mpya ya dawa ambayo inaweza kusaidia wagonjwa wa Ukimwi ambao wameshindwa kupata usaidizi wa dawa zingine. Kupatikana kwa dawa hii sasa kunaweza kusaidia watu hao kuwa buheri wa afya kwa kipindi kirefu,” alisema Dk. Debra Birnkrant, Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Dawa za Ukimwi katika Kituo cha FDA cha Kufanyia Utafiti wa Dawa.

Sunlenca ndio dawa ya kwanza ya kudhibiti virusi vya HIV kuwahi kuidhinishwa na shirika la FDA.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad