Diamond Platnumz Friji Aligandishi "Atoa Siri za Marioo"


Ki ukweli nimepokea Kwa Masikitiko makubwa Taarifa za Msanii wa Kundi la WCB kuvujisha Taarifa za Siri baina yake na msanii mwenzake
Najua unajiuliza Rais wa Wambea anamaanisha nini? Yes ninazungumzia statement aliyotoa Diamond Leo akimzungumzia msanii mwenzake anaefahamika Kwa jina la Marioo, Dai anasema Marioo alimfata na kuomba asainiwe na label ya WCB Kisha yeye akamjibu Nope we endelea kufanya mwenyewe kwani Tayari Muziki wako unafanya Vizuri, Ukifanya na Mimi radio nyingine watakua hawapigi ngoma zako, halafu Wasanii wa Wcb Zuchu Mbosso Lavalava wanapiga show kima cha chini Milioni 30 / 40 sisi tunapandisha standard, pengine wewe Marioo ushazoea kuokoteza show za Milioni 10 Or 15, ukija kwangu utakua huzipigi hizo, Akanielewa Vizuri mdogo wangu Marioo, akaniambia kweli Bigi, Dai akaendelea “ukihitaji msaada wowote Njoo Nikusaidie” mwisho wa kunukuu

Kwa statement hiyo ya mwisho kwa sisi Tuliosomea Cuba Tunasema Marioo amefedheheshwa na kudhalilishwa mbele ya Kadamnasi

Hakuna mtu anapenda mshahara wake utajwe hadharani

Najiuliza Haya mambo kama kweli waliyaongea kwa siri kitambo kwanini leo yanavujishwa? Kwann yasiendelee kuwa siri? Au ange chuja ya kusema public na mengine angeyaacha
Ina maana Dai hajui kama kuzungumza kauli hizi ata tafsirika kama anataka kumharibia biashara Mwenzake, kama alikua hajui kwa sasa Marioo ana biashara yake kubwa sokoni, ni album mpya sokoni inaitwa “The Kid You Know” ana Team Toto Bad inayoamini kuwa Mwaka huu 2022 Msanii huyu ameumaliza mwaka akiwa on Top,
Inawezekana Dai alikua na nia safi ila amekosea namna kuilezea vizuri,
Nawaza je Dai na U Legend wake kwenye Game, hivi ni kweli mpaka leo hajui madhara ya aina hii ya kauli yake dhidi ya msanii mwenzake yeyote? Kweli?
Je Yeye na wasanii wa Label yake watapenda kuzungumziwa vile na msanii mwingine?

Au Dai ana kinyongo?

Next time Dai afanye mazoezi ya Hotuba yake kabla ya kwenda nayo hewani, ili asitoe maboko ya namna hii kwani Wasanii wenzake wa bongoflava wanaweza kumshutumu kwa kutumia vibaya chombo chake au nafasi yake kuwashambulia kama hivi.

Kama Dai Ni Muungwana, atamuomba radhi Marioo Hadharani

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad