Diamond Platnumz Rasmi Aikataa Simba, Atamka Kwa Kinywa Chake Kumfuata Manara Alipo


Supastaa @diamondplatnumz sasa ni shabiki rasmi wa klabu ya mpira ya Yanga. Diamond ameweka wazi hilo alipokuwa akitangaza kuihama klabu yake ya zamani ambayo ni Simba.

@diamondplatnumz amesema amefikia maumuzi hayo kwa kumfuata rafiki yake Haji Manara alipo sasa. Amemtaja Haji kuwa ndiye aliyemvuta katika mambo ya mpira, hivyo alipo Manara na yeye yupo.

"Na mimi kama unavyonijua ulipo nipo. Hata ukienda Mtibwa na mimi nakuwa Mtibwa. Nlimwambia Onesmo (mlinzi wake) mimi nahama kwa sababu niliingia mambo ya kwenye Simba nilimfuata Haji na mimi sijui mpira. Haji kaondoka sasa mimi nabaki nafanya nini! kwa hivyo ulipo Manara na mimi nipo'' - Ameeleza @diamondplatnumz usiku wa jana kwenye birthday party ya Haji Manara.

Aidha, tayari klabu ya Yanga kupitia kurasa zake za mitandao ya Kijamii imemkaribisha Dimond Platnumz kwenye Chama la Wananchi.

Diamond Platnumz Rasmi Aikataa Simba, Atamka Kwa Kinywa Chake Kumfuata Manara Alipo 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad