Fei Toto Akimbilia Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa ya Michezo (CAS)


WAKATI Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likitoa taarifa iliyozua utata juu ya shauri la klabu ya Yanga dhidi ya kiungo Feisal Salum 'Fei Toto', upande wa nyota huyo kutoka Zanzibar umedaiwa umejipanga kukimbilia Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa ya Michezo (CAS).

Hata hiyo inaelezwa imekuja baada ya upande huo kuona hautatendewa haki baada ya TFF jana kutoa taarifa ikieleza Fei Toto ni mchezaji wa Yanga, huku ikieleza Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya shirikisho hilo iliyosikilizia shauri hiyo itatoa taarifa rasmi ya kesho Jumatatu.

Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa kiungo huyo fundi wa mpira aliyeamua kuvunja mkataba na klabu hiyo kwa kuilipa Sh 112 milioni ili awe huru kabla ya mabosi wake kuzirudisha fedha hizo, umesema tayari wameanza kukosa imani na TFF kwa taarifa iliyotolewa jana ikisainiwa na Ofisa Habari wa shirikisho hilo, Clifford Ndimbo.

Hata hivyo, kabla ya taarifa hiyo, Mwanaspoti lilipenyezewa kuwa, kamati iliyosikiliza shauri hiyo wajumbe wake wamegawanyika baadhi yao wakidaiwa kuweka unazi wao kwa klabu wanazoshabikia na kuwavuruga wengine waliotaka kusimamia haki na sheria kuhukumu shauri hilo.

Kamati hiyo yenye watu saba, lakini zaidi ya nusu wameegea upande mmoja, huku Fei akiweka bayana msimamo wake kwa wajumbe kwamba hawez8i kurudi Yanga hata kama wataamua hivyo na kwamba ataitafuta haki yake mbele zaidi kwani anaamini yeye sio mchezaji wa Yanga kwa sasa.

Inaelezwa tayari Fei, alikuwa anasubiri hukumu ya shauri hilo kabla ya kuamua kwenda CAS kwani tayari ameshaukabidhi mkataba wake kwa wanasheria wa kigeni kwa kuamini kuwa wana nafasi kubwa ya kushinda shauri hilo hata kama TFF itaamua kupindisha kama ilivyotoa taarifa ya jana.

"Fei ameshaweka msimamo wake, hawezi kurudi Yanga kwani ameshamalizana nao na juzi kwenye shauri alisisitiza hilo. Kwa sasa anasubiri hukumu itakayotangazwa Jumatatu, ili achukue hatua zaidi," kilisema chanzo hicho kilichohoji pia taarifa ya TFF kukanganya kwa kusema kiungo huyo ni mali ya Yanga wakati maamuzi ya shauri hiyo hayatolewa na kamati ili kujua ukweli ulivyo.

Kiungo huyo aliyesajiliwa na Yanga mwaka 2018 kutokea JKU, japo alikuwa akielekeza Singida United, alipotafutwa jana kwa njia ya simu alijibu kwa kifupi; "Kwa sasa niacheni, siwezi kusema lolote."
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad