Harmonize Aanika Hadharani Majibu yake ya Virusi vya Ukimwi



Supastaa wa Bongo Fleva, Harmonize ambaye hivi karibuni aliposti picha yake  na mpenzi wake mpya, sasa ameanika ghafla kwa mashabiki wake alipochapisha majibu yake ya vipimo vya VVU.


Kwa wale wanaojali kuhusu hali ya msanii na staa wa bongo Harmonize ya virusi vya Ukimwi  sasa wanamajibu ya wazi baada ya msanii huyo kuanika matokeo yake mitandaoni.


Harmonize, ambaye alishiriki picha yake  na mpenzi wake mpya wiki mbili zilizopita, alichomoa kadi ya ghafla kwa mashabiki wake alipochapisha majibu yake ya vipimo vya VVU.


Harmonize alichukua nafasi hiyo kuwanyamazisha wakosoaji wake wote waliohoji kupungua kwake kwa kuhofia kuugua.


Mwanamuziki huyo mwenye utata alifunguka kuhusu matokeo ya kipimo cha VVU alichochukua nyumbani kwake kwa kutumia kifaa cha kujipima.


Ingawa chapisho hilo lilikuwa hatua ya kusifiwa, lilizua hisia tofauti kutoka kwa mashabiki na wakosoaji, na kujitokeza hadharani kupima VVU baada ya kuachana na aliyekuwa mke wake Faridah Kajala.


Ufichuzi wake Harmonize unajiri siku chache baada ya kumfokea Rayvanny mitandaoni kwa kuanika uchi wake.


Harmonize amekuwa akivuma mitandaoni kwa ajili ya matendo yake tofauti,kutoka kuridhisha Kajala warudiane hadi kukashifiana na Rayvanny mitandaoni.


Vita hivyo vilichukua mkondo mwingine wakati wawili hao walianza kuingiliana katika maelezo ya kibinafsi na kujilinganisha katika suala la mafanikio.


"Ulilipa Wasafi 600M ukalia kwenye mitandao ya kijamii,kama hujui nililipa Wasafi bilioni 1.3 ukihisi naongeza sifuri fatilia au nenda BASATA ukaulize na umeona nimeongea wapi? pesa sio kitu kwangu kikubwa ni heshima ndio kitu ninachokithamini ukiona siku nimeongea ujue nimekosewaheshima kupita kiasi,"Aliongea Rayvanny.


Bosi huyo wa Lebo Next Level Music alimkumbusha mwenzake huyo wa Konde Music Worldwide kuwa bila bosi wao wa zamani Diamond Platnumz hangekuwa ameweza kufika kilele ambacho amefanikiwa kufika kwa sasa.


Pia alijigamba kuwa yeye ni bora zaidi kuliko Konde Boy katika masuala ya ubunifu na utayarishaji wa muziki.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad