Harmonize na Rayvanny Walikuwa Hawapatani Toka Wakiwa WCB, Wapigana Vita Hadharani


Mbosso amewahi kufunguka kwamba HARMONIZE hakuwa Mshikaji wake kipindi alipokuwa WCB. Hii inafikirisha sana, inakuaje watu wapo kwenye Label moja then wanashindwa kuwa Washikaji?

Hii inaleta picha kwamba Hata Rayvanny ni muongo, wakati Harmonize ameondoka WCB, Rayvanny alifunguka kwamba Harmonize alikuwa mshikaji wake na alikuwa anamtetea sana wakati akionewa hapo WCB. Inaonesha watu hawa walikuwa wana ushikaji wa kinafiki sana.

Kama wangekuwa washikaji kweli, siku ile Airport Harmonize alisingevujisha Voice note za Rayvanny akiwazungumzia Vibaya WCB. Naamini zile Voice note zilimchonganisha na WCB ndio maana si muda mrefu Rayvanny pia aliondoka.

Pia Harmonize alitaka kumchongea Rayvanny afungwe miaka 30 kisa anatembea na Mwanafunzi (Paula). Mbaya zaidi Rayvanny akavujisha Mkonga wa Harmonize, ingawa yeye mwenyewe anasema hakuvujisha, Bali walivujisha wale ambao Harmonize alikuwa anawatumia huo mkonga. Haya yote yanaonesha Rayvanny na Harmonize walikuwa na Ushikaji wa Kinafiki walipokuwa WCB.

Hii vita yao sasa hivi inaonesha Jinsi gani hawapendani. Ilibidi wachukie sehemu waliyotoka, wala sio wao kwa wao. Hivi umeona wapi watoto wanaonewa kwenye Familia, then wanakimbia, watakapokimbilia tena waanze kuchukiana?

Cha msingi Harmonize na Rayvanny wawe kitu kimoja, hakuna haja ya kuvimbiana, ukweli unajulikana kwamba wote hawana hela, watafute hela wawe kama Diamond.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad