Hatimaye Makamu wa Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Akubali Uteuzi wa Rais na Kuapishwa


Dinah Elias Mathamani aliyeteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan ameapishwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye leo January 31 kuwa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza iliyopo Mkoani Kigoma.

Kuanzia juzi January 29,2023 zilisambaa taarifa mitandaoni kwamba DC huyo ambaye alikuwa Makamu wa Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na wenzake wamekataa uteuzi, DC Dinah amesema taarifa hizo zilikuwa sio za kweli kuhusiana na yeye kukataa uteuzi huku akisema anawatafuta Waandishi wa Habari waliokuwa wanachafua jina lake bila ya kupata habari za uhakika kutoka kwake.

"Mimi baada ya kuona jina langu nilimshukuru Mungu na Rais kwa kuniamini lakini baadaye nikaanza kuona kwenye mitandao kwamba nimekataa uteuzi na sijui chanzo cha habari hiyo Waandishiwalitoa wapi, niwaombe tu Waandishi wanapotaka kutuma taarifa kwa umma msilete taharuki kwa jambo ambalo hamna uhakika nalo"

"Mimi mwenyewe nilisikitika kuona na Mimi jina langu limo kuona kwamba nimekataa wakati sio kweli na hata hivyo hao Waandishi nawatafuta ili wanieleze kwa nini waliniandika jina, kibinadamu inatakiwa waombe radhi"

Itakumbukwa Rais Dkt.Samia January 25 mwaka huu alifanya uteuzi wa Wakuu wapya wa Wilaya 37, kuwahamisha vituo vya kazi Wakuu wa Wilaya 48 na wengine 55 kubakia kwenye vituo vyao.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad