Hatimaye ndoa ya Dk Mwaka na Mkewe Queen Masanja imevunjwa Rasmi leo


Hatimaye ndoa ya mtaalamu wa tiba mbadala, Juma Mwaka maarufu Dk Mwaka na mkewe Queen Masanja imevunjwa rasmi leo Jumatano, Januari 25, 2023.

Ndoa hiyo imevunjwa baada ya kikao cha Kamati ya Masheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam chini ya mwenyekiti wa masheikh wa mkoa, Alhadi Mussa Salum kuketi kwa dharura na kuridhia maombi ya Queen kutaka apewe talaka.

“Ndoa hii imepoteza malengo makusudia hakuna upendo wala maelewano baina yao hadi sasa zaidi ya mwaka mmoja sasa,” Shekh wa Mkoa wa Dar akizungumza na Wanahabari.

Itakumbukwa, mapema Jumatatu ya wiki hii, Queen alizungumza na Wanahabari na kueleza mengi kuhusu ndoa yake ikiwemo pia kufika Bakwata na kuwa akizungushwa kupewa Talaka yake licha ya kuwa sheria za dini zinaruhusu na kuna utaratibu wake.

Pia Queen alieleza kwamba ameamua kuachana na Dk Mwaka baada ya kutoridhishwa na baadhi ya mambo ambayo yalikuwa yanaendelea kwenye ndoa yao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad