Anerlisa ameamua kumwaga petroli kwenye moto, ameachia meseji za Ben Pol ambazo alikuwa akimtumia kupitia WhatsApp tangu mwishoni mwa mwaka Jana. Jumbe hizo ambazo zimeanikwa hadharani na mtandao wa Kenya (@mpashogram), zinaonesha Ben Pol akimkumbusha Anerlisa matukio ya maisha yao na kumueleza hisia zake, akitaka warudiane.
Sakata hili lilianza baada ya Ben Pol kufanya mahojiano na Mtangazaji Millard Ayo, ambapo alikaririwa akisema hakuwahi ku-enjoy ndoa yao na ilikuwa ya mapicha picha tu. Anerlisa alitoka hadharani kupitia insta story na kumuonya Ben Pol asiongelee masuala ya mahusiano yao mitandaoni, vinginevyo atamuanika!
Soma Meseji Alizovujisha Anerlisa