Ingawa Kalipa Mabilioni ya Pesa Kwa WCB, Rayvanny Ashindwa Kumlipa Hata Shilingi 50 Producer Aliyemtoa


Mtayarishaji wa muziki nchini, Zest amefunguka kutolipwa hata kiasi cha Sh. Elfu 50 na mwanamuziki Rayvanny kufuatia kazi zote alizowahi kumfanyia ilihali mkali huyo ameweza kulipa Bilioni 1.3 ili kumalizana na uongozi wake wa zamani.


@zest_soundkiller ambaye alikuwa akifanya kazi na msanii Rayvanny kipindi cha nyuma, ameshangazwa na jambo hilo akihoji producers sasa wanatakiwa kujitazama, wanasindikiza sana watu kwenye utajiri.


"Dogo kalipa 1.3 Bilion kuondoka Wasafi lakini anashindwa kunilipa ata elfu 50 ya kazi zote nilizowahi kumrecord, kuna namna Producers tunatakiwa kujitazama tunasindikiza sana watu kwenye utajiri.


"Sasa naona ni muda sahihi wa kufwatilia haki zangu zote 2023 nataka malipo ya ngoma zote nilizowahi kutengeneza maana mpaka sasa pesa zinaingia kupitia kazi nilizowahi kuzifanya na sioni kitu". - ameeleza Zest kwenye ujumbe wake Instagram.


Ingiwa Kalipa Mabilioni ya Pesa Kwa WCB, Rayvanny Ashindwa Kumlipa Hata Shilingi 50 Producer Aliyemtoa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad