Juma Lokole akiri kulipiwa kodi na Diamond, awaumbua wanaokataa, ni zaidi ya 50 “Bora Gigy kajisema mastaa ni wengi”
Mtangazaji wa Wasafi Fm @jumalokole20 amedai @diamondplatnumz akipata matatizo kuwa watu wangi wataumia kwani anategemewa na watu wengi ambao ni nje na ndugu wa damu.
Kichefuchefu amedai list yake kwa harakaharaka ina watu zaidi ya 50 nje ya ndugu zake wa damu wakiwemo mastaa wa muziki na filamu pamoja na marafiki.
Amesema yeye na @officialbabalevo ni miongoni mwao ambapo amedai wengi wanaogopa kujitaja.
Hatua hiyo imekuja baada ya @gigy_money_og kudaiwa kuomba kodi kwa Diamond katika mazingira sio mazuri na kuzua gumzo.