Kijana Adai Kudhurumiwa Fedha za Urithi na Muna Love

 


Kwenye mahojiano ya hivi karibuni, kijana anayedaiwa kuwa alikuwa mtu wa karibuni wa Muna love na wameishi wote kwa miaka kadhaa kama mtu na dada yake amesema anamdai Muna Love kiasi cha pesa za Kitanzania milioni tatu ambazo alizipata baada kuuza nyumba yao ya urithi baada ya wazazi wao wote wawili kufariki.


Prince Feyz amesema nyumbani kwao wamezaliwa wawili tu yeye na dada yake, baada ya wazazi wao kufariki dada yake alimshauri wauze nyumba yao na baada ya kuafikiana waliiuza kwa milioni kumi ambapo waligawana milioni tano tano.


Baada ya kugawana Feyz anasema yeye hakuwa na account ya Bank akaamua kumkabidhi Muna Love amuwekee maana alimuamini kama dada yake kutokana na walivyokuwa wakiishi, lakini sekeseke lilikuja baada Feyz kuzitaka pesa zake ambapo Muna alionekana kuzitumia zile pesa na kuanza kumpa kidogo kidogo.


Amesema alilipwa milioni mbili tu, nazo alilipwa kwa awamu nyingi na hiyo milioni tatu iliyobaki Muna amegoma kumlipa kabisa na kum'block juu, kijana huyo amesema anapitia wakati mgumu sana kwa sasa ilihali Muna amezikumbatia pesa zake za urithi na siyo kwamba hana uwezo wa kumlipa ila ameamua tu kutomlipa.


"Naumia kwasababu namuona anaenda Uturuki kufanya sajari lakini pesa zangu imekuwa ngumu kunipa nacnikiwaagiza watu wake wa karibu anawambia ameshanilipa, siwezi kumsamehe kamwa hadi nilipwe pesa zangu, hata akidondoka mbele yangu maiti yake nitaizuia isiondoke hadi pesa yangu irudi, maana kwa sasa naishi maisha magumu sana".


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad