Kiungo Wa Zamani Wa Zambia Auawa Na Mbwa Wake Watatu, Mkewe Afunguka



Nyota wa zamani wa Chipolopolo ya Zambia, Philemon Mulala aliumwa na mbwa wake watatu nyumbani kwake Lichtenburg Afrika Kusini alipotoka nje kuchunguza kwanini mbwa hao walikuwa wanabweka sana baada ya umeme kukatika. Msemaji wa polisi, Sam Tselanyane, alisema kuwa mke wake aliwaambia kwamba alisikia mbwa wakibweka lakini hakujishughulisha na kwenda kuangalia ni nini kilikuwa kibaya kwani mbwa hao mara kwa mara walikuwa wakiwabwekea watembea kwa miguu na magari yaliyokuwa yakipita.


“Baada ya umeme kurudi , aliingia ndani ya nyumba hiyo akimtafuta mumewe lakini hakumpata, baada ya kuendelea na upekuzi, mwanamke huyo alimuona mumewe akiwa amelala nje kwenye bustani. Kisha akatoka nje kupeleleza kulikoni, na akagundua mume wake alikuwa hatikisiki baada ya kuumwa na mbwa wao watatu.”


Mamlaka zimewaondoa mbwa hao wawili ambao ni ‘Cross breed” ya Pitbul na mbwa wa tatu hajulikani asili yake ila anasemekana kuwa mkali.


Mulala alihamia Afrika Kusini kuichezea klabu ya Kaizer Chiefs mwaka wa 1988. Pia alichezea Cape Town Spurs na Lenasia Dynamos.


Shirikisho la soka la Zambia (FAZ)limetoa taarifa ya kuomboleza kifo cha Mulala likisema alikuwa sehemu ya kikosi cha Zambia cha mwaka 1984 kilichoshinda Kombe la East and Central Africa Challenge chini ya ukufunzi wake kanali Brightwell Banda.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad