Zaidi ya miaka tisa imepita tangu Daimond Platnumz aingie kwenye masikio ya watu na wimbo wake wa Nitarejea.
Binafsi wimbo huo uliwafanya watu wajue kuna msanii anaitwa Diamond. Wimbo ulikuwa na kila sababu ya kupendwa kutokana na ujumbe wake, akimueleza mke wake kwamba anakwenda kutafuta mjini, huku kijijini akichoshwa na maisha magumu, kilimo bila mvua.
Hakika wimbo huo ulikuwa na ujumbe kwa pande zote mbili wanawake na wanaume, kwamba Wanaume wanatakiwa kupambana kwaajili ya familia zao na wanawake wawaombee ili wafanikiwe waje kuishi na familia zao.
Kwenye wimbo huo Mondi alipewa ushauri na mkewe kwamba hasije akasahau kwamba ameacha mke na watoto kijijini mara baada ya kufanikiwa.
Mondi akaja mjini na akafanikiwa kweli, wala hajamsahau mkewe maana hata kwenye shoo ya mwishoni mwa mwaka 2022 kwenye jukwaa alionekana akiwa na msanii Hawa aliyeimba naye wimbo huo wa Nitarejea.
Lakini mapema mwaka huu amekuja na wimbo wa Yatapita, moja kati ya wimbo wenye ujumbe mkubwa sana, hasa kuwataka wanawake kuwa wavumilivu kutokana na ugumu wa maisha, hivyo ipo siku yatakwisha na kusahau magumu waliyoyapitia.
Jumatano ya tarehe 25, Januari hii Mondi akaachia video ya wimbo huo, hakika kuna uhalisia mkubwa kile kilichoimbwa na kulichopo ndani yake, hongera sana Mondi kwa video kali yenye uhalisia.
Wakati anaachia wimbo wa Nitarejea, wengi waliamini ni ngumu kuja kufanya wimbo wenye ujumbe mkubwa kama huo, lakini kwa Yatapita ni wazi kwamba amerejea kwenye uhalisia wake wa kuandika kwa ajili ya maisha ya watu wengi kwenye jamii.
Yatapita awewataka wanawake wengi kuamini kuwa maisha yanabadilika, hivyo wanatakiwa kuwa wavumilivu hayo maisha Yatapita na wataishi kama wanavyoishi wengine waliobarikiwa.
Mondi anatuonesha kuwa bado ana njaa ya mafanikio ya muziki japokuwa tayari amefanikiwa, lakini anatoa ujumbe hata kwa wasanii wengine kuwa muziki bado unawadai.
Kuna vitu vingi vya kuimba kwa ajili ya jamii na ujumbe ukafika na kuwapa nguvu na kuwainua vijana kama ilivyo kwa Mondi na nyimbo zake Nitarejea, Yatapita na nyingine nyingi.
@badimchomolo