Maelfu wamiminika kwa Mtume Mwamposa, yeye asema...



Dar es Salaam. Maelfu ya waumini walifurika viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ibada ya mkesha wa mwaka mpya 2023.

 Ibada hiyo ilifanyika katika Kanisa la Inuka Uangaze, usiku wa kuamkia leo Jumapili, Januari 01, 2023 na kuongozwa na Mtume Boniface Mwamposa.

Siku chache zilizopita wafuasi wa Mtume Mwamposa waliujaza Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam na wengine kubaki nje kutokana na wingi wao katika Uwanja wa Mkapa,Dar es Salaam.

Mwamposa, maarufu ‘Buldoza’ wa Kanisa la Arise and Shine (Inuka Uangaze), usiku wa kumkia Disemba 18, 2022 aliendesha mkesha aliouita “Vuka na Chako Kabla ya Kuvuka Mwaka” ulioweka rekodi ya mahudhurio kwa kuujaza uwanja huo unaoweza kuchukua mashabiki 60,000 waliokaa, huku wengine wanaokadiriwa 20,000 wakikaa kwenye korido.


Mwananchi Digital iliyofika na kuweeka kambi uwanja wa Tanganyika Packers ilishuhudia maelfu ya waumini wakiwa uwanjani hapo huku wengi wao wakiwa wamepanga foleni ya kununua mafuta, maji na udongo.

Baadhi ya wauminj walisema wengi wao wamefika uwanjani hapo tangu saa nane mchana wa jana Jumamosi  ili kuwahi nafasi huku baadhi yao wakitoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam.

"Nabii Mwamposa ana waumini wengi, mimi nimefika hapa toka saa nane ili kuwahi nafasi lakini pia kupata mafuta ya upako," alisema Elisia mmoja wa wawaumini


Gipson Haule, alisema alifika uwanjani hapo saa kumi jioni lakini alikuta umati wa watu, hata hivyo alibahatika kupata mafuta baada ya kukaa kwenye foleni hadi saa moja usiku.

Hadi kufikia saa nne usiku ibada ilikuwa haijaanza kutokana na hitilafu ya vyombo huku waumini wakiendelea kuimba.

Ilipofika saa 5:15 usiku Mtume Mwamposa aliiwasili uwanjani hapo na kuongoza maombi hadi ilipofika saa 6:00 usiku ambapo watu walianza shamrashamra zikiambatana na fataki.

Katika mahubiri yake Mwamposa alisema amefungua Hoteli pamoja na eneo la kusali lililoko mkoani Mbeya, kwa wale watakaohitaji wanakaribishwa.


"Nimeshafungua Hoteli na sehemu ya kusali iliyopo Mbeya mlimani kwa wale wahaohitaji wanakaribishwa, baada ya kuvuka na chako," alisema Mwamposa.

Katika mahubiri yake, Mtume Mwamposa alitangaza ujumbe wa mwaka 2023 katika mkesh huo akisema mwaka 2023 ni mwaka wa baraka za kuongezeka na kuzindishwa. Utatembea na jeshi lisilo onekana. Utatawala na kumiliki.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad