Mazito Mke Wa Manara Yaibuka Kuendelea Kumhudumia Hadi Amalize Eda Yake




WENGI wanadhani kwa kuwa dini ya Kiislamu imeruhusu talaka basi jambo hilo laweza kufanyika kimchezomchezo; wanazuoni wanasema “La hasha.”


Hivi karibuni kumekuwepo madai kuwa aliyekuwa msemaji wa Yanga Haji Manara amemtaliki mkewe wa pili; Rushaynah Athumani.


Ijumaa lilimtafuta Shehe Ahmed Kandauma kutoka taasisi ya dini ya Kiislam IRSHAD ya Temeke jijini Dar ili kupata ufafanuzi wa nini anachotakiwa kukifanya mwanamke huyo baada ya kupewa talaka ambapo alibainisha mambo yafuatayo:


“Talaka moja kwa tafsiri za wazee ni talaka ya hekima ambayo inampa mume na mke wasaa wa kujitathimini juu ya makosa yaliyowatenganisha.


“Kwa mwanamke hawi huru baada ya kupewa talaka, ni wajibu wake kukaa eda hadi siku tisini.


Wakati huyo wa eda umewekwa maalumu pamoja na mambo mengine ni kuangalia kama alipotoka kwenye ndoa hakuna na ujauzito kutoka kwa mumewe.


“Kwa muktadha huyo mwanamke aliyachika kwa talaka moja hatakiwi kukutana kimwili na mwanaume mwingine au kuolewa katika ndoa nyingine.


“Kwa upande wa mume jukumu la kuendelea kumhudumia mkewe huyo litaendelea hadi amalize eda yake.


“Na wazee wa dini wanasema ni hekima kama mwanamke huyo atakaa eda kwenye nyumba ya mumewe; inaweza isiwe chumba kimoja lakini hata chumba kingine hilo linapendeza zaidi,” alisema Shehe Kandauma.


Kwa mujibu wa machapisho ya kidini ambayo Ijumaa limeyaperuzi yanaelekeza kuwa endapo siku tisini zitapita badi mke atakuwa na ruhusa ya kuolewa na mumuwe akitaka kumrejea itabidi amuoe kwa kumposa mahari mpya.


Aidha inadokezwa kuwa endapo mume na mke wakivunja eda kwa kukutana kimwili basi eda hiyo itakuwa imekoma na maisha ya ndoa kuendelea kama yalivyokuwa awali.


Kuhusu madai ya Manara kuoa na kuacha Shehe anasema kuacha mke si jambo jema lakini inapobidi mwanaume hafungwi na sheria na kwamba anaweza kuacha na kuoa mwanamke mwingine.


Tangu uwepo wa taarifa za Manara kutengana na mkewe kumekuwa na kelele nyingi kwenye mitandao ya kijamii huku nyingi kati ya hizi zikimlaume Manara kwa kuyaanika maisha yake na wakeze kwenye mitandao ya kijamii.


“Sasa ndiyo nimesikia anasema hataki kuzungumzia ishu ya ndani ya familia, lakini ni Manara huyuhuyu amekuwa akiposti picha kwenye mitandao ya kijamii akiwa na wake zake, dini anazua mke wa mwislamu kunadiwa kwani ni pambo la mumewe siyo vinginevyo,” aliandika komenti mtu mmjoja kwenye Instagram.


Mengi yasiyokuwa na ushahidi yanasemwa kama kisa cha Manara kutofautiana na mkewe ambapo Ijumaa limebaki kuyafumbata kusubiri ukweli utoke kwa wahusika.


Maana tangu sakata lichipuke Manara amekuwa mkimya kulitolea ufafanuzi na kuacha mambo ya mitandaoni yaendelee kupokea habari zisizokuwa na ushahidi.


Na Mwandishi Wetu, GPL

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad