Mbowe awaomba radhi Wanawake Kwa Kuwaita Mademu



Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe awaomba radhi kutokana na kauli yake aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa mkutano wa hadhara uliofanyika Jijini Mwanza, asema haikuwa ya staha ndio maana chama hicho kinaomba radhi.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amewaomba radhi Watanzania kutokana na kauli yake aliyoisema kupambana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) haihitaji sayansi ya kidiplomasia bali pia inahitaji ushawishi kama vile ‘kutongoza demu.’


Mbowe ambaye ni kiongozi wa zamani wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni (KUB), alitoa kauli Jumamosi ya Januari 21, 2023 wakati akihutubia mkutano wa kwanza wa hadhara wa chama hicho, uliofanyika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.

Mara baada ya kauli hiyo, kuliibuka mijadala na baadhi wakimtaka kuomba radhi ambapo leo Jumatatu Januari 23, 2023 akiwa katika mwendelezo wa ziara yake ya mikutano ya hadhara katika uwanja wa Shamba la Bibi wilayani Tarime, mkoani Mara akikaribia kumaliza hotuba yake, Mbowe ametumia nafasi hiyo kuuomba radhi kwa umma kutokana na kauli hiyo.

“Kuna jambo moja nataka kulisema, nililizungumza katika mkutano wa siku mbili zilizopita, nikazungumza katika kujenga hoja yangu. Nikawazungumzia mama zetu, kama ‘mademu’ kuna watu imewakwaza kidogo.

“Naelewa haikuwa lugha ya staha, lakini kiongozi mstaharabu haogopi kuomba radhi wale ambao walifikiri nilitumia lugha ile vibaya nawaomba radhi sana…Mama zangu nawapenda na Chadema inawapenda kina mama na hakiogopi kuomba radhi, kinapoona kimejikwaa mahali,” amesema.

Mbowe alitumia jukwaa hilo kuwaomba radhi wananchi, akiwataka kukisamehe chama hicho, akisema viongozi wa Chadema ni watu waungwana wanaowapenda kina mama na wanaamini katika harakati zao na watahakikisha wanawabeba ili kufikia katika harakati za usawa wa kijinsia na kuheshimiana katika Taifa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad