Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na jarida la African Fact zone kuwa mchezaji anayeongoza kulipwa zaidi katika bara la Afrika anatoka katika klabu ya Al ahly ya Misri ambaye ni Ali Maaloul akilipwa ($1.5 million) sawa na Tsh 3,502,500,000/= kwa mwaka huku akifuatiwa na raia wa Arika Kusini akicheza Al ahly Percy Tau ambaye analipwa ($1.2 million) |sawa na Tsh 2,802,000,000/=
Kwa maana hiyo mshahara wa mchezaji anayeongoza kulipwa zaidi Afrika kwa ligi za ndani ni Ali Maaloul ambaye anapokea bilioni 3.5 za Kitazania kwa Mwaka.
Mshahara wake kwa mwezi utakuwa milioni 291,875,000/=, huyo anaongoza kwa ligi zote Afrika ila anayeongoza kwa ligi kuu Tanzania ni Aziz Ki anayechezea klabu ya Yanga analipwa milioni 27 za Kitazania kwa mwezi kwa Mwaka ni sawa na milioni mia tatu huku anayeongoza Afrika akipokea bilioni 3.5 za Kitazania kwa mwaka huku kwa mwezi akilipwa milioni mia mbili tisini na moja.
Tofauti ya mshara ni mkubwa sana unahisi kuna mchezaji kutoka ligi ya Misri anaweza kuja kuchezea Tanzania mwenye mshahara wake A list ya wachezaji wanaolipwa Afrika??
Unahisi ligi yetu ipo nafasi ya ngapi kwa kulipa wachezaji barani Afrika??