Dodoma. Mchezaji wa timu ya vijana U 17 ya Singida Big Stars Mohammed maarufu Banda amefariki mazoezi mara baada ya kugongana na mchezaji mwenzake wakati wakigombea mpira wa juu.
Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Singida (Sirefa), Hamis Kitila amethibitisha kutokea kwa kifo hicho.
Mwenyekiti huyo amesema mchezaji huyo amefariki leo asubuhi wakati timu ya U17 ikifanya mazoezi katika uwanja wa Magereza mkoani Singida.
"Ni kweli walikuwa kwenye mazoezi asubuhi jina la marehemu anaitwa Mohammed hili Banda ni la utani lakini anajulikana zaidi kwa jina hilo," amesema Kitila.
Kitila amesema kwa sasa vikao vinaendelea na watatoa utaratibu baadae nini kinachofuata.