Msanii wa singeli nchini Meja Kunta ameweka wazi kuwa kwa sasa hayupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na aliyekuwa mpenzi wake Tunda.Hii imekuja mara baada ya Meja Kunta kuulizwa na moja kati ya watu waliokuwa wakimuuliza maswali kupitia Instastory yake, mtu huyo alimuuliza kama bado ana uhusiano wa kimapenzi na Tunda na Mejakunta akajibu 'HAPANA'.
Ikumbukwe Meja Kunta na Tunda walikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi hadi kufikia hatua ya kuvalishana pete ya uchumba.
Meja Kunta Amwangana na Mrembo Tunda