Meli ya mizigo ya Tanzania iitwayo Anil imepinduka katika bandari ya Assaluyeh Kusini mwa Iran Siku ya Jumanne, Januari 24 kutokana na mpangilio mbaya wa Makontena kwenye bodi.
Ajali hiyo imetokea katika Bandari inayohusika na kemikali za petroli na gesi zinazozalishwa nchini Iran iliyopo kilomita 950 kusini mwa Tehran.
Katika taarifa iliyotolewa na IRNA, tovuti rasmi ya habari ya Iran, ilifichuka kuwa wafanyakazi wa Meli waliokolewa na kupelekwa kwenye eneo salama na timu ya uokoaji. Maelezo zaidi bado hayajatolewa.
Biashara ya Shehena ya kila mwaka kati ya Tanzania na Iran ni chini ya dola milioni 100 lakini mauzo ya nje na uangizaji umepungua tangu tangu Marekani ilipoweka vikwazo kwenye mafuta na benki ya Iran.
Meli hiyo ilikuwa na wafanyakazi 12 na wametoka salama.