Wadau wa madini ya Tanzanite wameiomba serikali kutumia taasisi zake kudhibiti wanaopotosha kwamba madini hayo yanatoroshwa licha ya udhibiti katika uchimbaji na uuzaji.
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa Chama cha Wanunuzi na Wauzaji Madini Tanzania (Tamida), Sammy Mollel amesema athari za kuendelea kufumbia macho upotoshaji huo ni kubwa.
Amesema wadau wa madini wamesikitishwa na taarifa hizo na amewataka Watanzania kutoa ushirikiano kuwabaini wanaoeneza taarifa hizo.
“Tangu kujengwa kwa ukuta katika eneo la Mirerani mwaka 2017 na kufungwa kwa mitambo ya kielektroniki ya ulinzi kumesaidia kuondoa mianya ya utoroshaji wa madini na kwa hali inayoonekana hapa hakuna utoroshaji unaoweza kufanyika kutokana na udhibiti mkubwa uliopo, taasisi zote za serikali zipo, mifumo yote imekamilika na inafanya kazi, huo utoroshaji unaodaiwa unafanyika wapi na kwa njia gani?"
"Kama mtu ana uhakika na taarifa hizo ni vizuri akatoa ushirikiano kwa kutoa ushahidi namna madini hayo yanatoroshwa pamoja na kuonyesha mianya yote ili wanaohusika waweze kuchukuliwa hatua na sio kutoa taarifa za kupotosha ambazo kwa tafsiri nyingine zinadhalilisha kazi yote iliyofanyika na uwekezaji wote uliopo," amesisitiza.
Naye ofisa madini mkazi Mirerani, Menard Msengi amesema serikali imeweka ulinzi wa kutosha na mazingira mazuri kuanzia kwenye miradi hadi kufika sokoni katika kuhakikisha sheria zote zinafuatwa na kwa ulinzi uliopo suala la utoroshaji haliwezi kufanyika hata kidogo.
Naye mwenyekiti wa chama cha wanunuzi wadogo wadogo wa madini Tanzania (Chamata), Jeremia Kituyo amesema taarifa za kuwepo kwa utoroshaji wa madini zinasababisha washindwe kufanya biashara kwani zinawaondolea uaminifu kwa wateja.
"Tunasikitika sana na matamko yanayotolewa yasiyo na ushahidi kwamba madini yanatoroshwa..., ni za kutuvunja moyo na kuharibu sura ya biashara ya madini nchini," amesema.
Mhandisi migodi kutoka kampuni ya Franone Mining, Benezet Karyuka amesema uwepo wa ukumewasaidiauta umewasaidia ulinzi.