Kupitia ukurasa wake wa Instagram msanii huyo wa Bongo Fleva @iambenpol amepost barua ya wazi akimuomba msamaha Ex-wife wake @anerlisa kutoka nchini Kenya kwa kile alichozungumza.
Akifanyiwa mahojiano na mtangazaji kutoka Clouds @millardayo @iambenpol alieleza kuwa hakuwahi kufurahia ndoa yake na @anerlisa
Baada ya mahojiano hayo @anerlisa alimuomba @iambenpol aache kumzungumzia na akaahidi endapo ataendelea basi atapost meseji zake kwani anqchoongea kwenye media ni tofauti na anachomtumia.
@iambenpol kwenye barua yake hiyo ya wazi ameeleza kuwa lengo lake lilikuwa kueleza namna alivyopitia magumu na kuathirika kisaikolojia hakuwa na lengo na kumuumiza Ex-wife wake.