Mtoto wa El Chapo akamatwa Mexico | Son of Mexican drug lord "El Chapo" arrested



Ovidio Guzman ‘El Raton’ ambaye ni mtoto wa muuzaji maarufu wa dawa za kulevya nchini Mexico, Joaquin ‘El Chapo’ Guzman amekamatwa ikiwa ni siku chache kabla ya Rais wa Marekani Joe Biden kuzuru nchini humo. 

Dar es Salaam. Vikosi vya usalama nchini Mexico vimemkamata mtoto wa kiume wa muuzaji maarufu wa dawa za kulevya Joaquin ‘El Chapo’ Guzman na kusababisha vifo vya wanajeshi watatu katika harakati za kumuweka chini ya ulinzi.

Taarifa iliyotolewa na shirika la habari AFP Januari 5 imesema kuwa, Ovidio Guzman (32), aliyepewa jina la utani ‘El Raton’ alinaswa katika mji wa Kaskazini-Magharibi wa Culiacan na kusafirishwa hadi Mexico City kwa ndege ya kijeshi.


Taarifa iliyothibitishwa na Waziri wa Ulinzi, Luis Cresencio Sandoval alisema wamemkamata kijana huyo baada ya kumsaka kwa miezi sita, ikidaiwa anasaidia kuendesha shughuli za baba yake tangu aliporejeshwa Marekani mwaka 2017.

Marekani ilikuwa imetoa zawadi ya hadi dola 5 milioni kwa atayekuwa na taarifa zitakazowezesha kumkamata Ovidio Guzman, ikimtuhumu kuwa mhusika mkuu katika kundi la Sinaloa.

Milio ya risasi na moshi ulitikisa Culiacan baada ya kukamatwa, ambayo inakuja wakati Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador anajiandaa kumkaribisha Biden wiki ijayo atakuwa na mkutano wa kilele wa viongozi wa Amerika Kaskazini huko Mexico City ambapo usalama unatarajiwa kuwa ajenda kuu.

Takriban watu 18 walijeruhiwa katika ghasia hizo, gavana wa jimbo la Sinaloa Ruben Rocha alisema, huku ndege zaidi ya 100 zikisitisha safari zake katika jimbo hilo.

Vilevile shule katika mji Sinaloa zililazimika kufungwa kutokana na ghasia hizo ambapo kundi la mtoto huyo wa El Chapo waliamua kujibu mapigo wakishambulia kwa risasi ndege ya abiria iliyokuwa inajiandaa kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Culiacan, lakini hakukuwa na majeraha, shirika la ndege la Aeromexico lilisema.

El Chapo anatumikia kifungo cha maisha nchini Marekani kwa kusafirisha mamia ya tani za dawa za kulevya nchini humo katika kipindi cha miaka 25.

Son of Mexican drug lord "El Chapo" arrested

Ovidio Guzmán, the son of infamous Mexican drug lord ""El Chapo,"" was arrested Thursday in a military raid in Mexico. Guzman is wanted by the U.S. for alleged drug trafficking.

 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad