Mwenyekiti wa Klabu ya Simba "Basi la Simba Limeuzwa na Sio Bovu"


Mwenyekiti wa Klabu ya Simba ambaye anamaliza muda wake, Murtaza Mangungu amekiri kuwa basi la timu hiyo limeuzwa na sio bovu kama inavyoelezwa.

Klabu hiyo ambayo imekuwa ikitumia basi dogo aina ya ‘Coaster’ kwa muda sasa huku basi hilo likiwa halionekani na taarifa za awali kusema kuwa limepata hitilafu, sasa limethibitika kuuzwa.

“Nashushiwa lawama ambazo sio zangu, basi la Simba limeuzwa mimi nikiwa sipo kwenye uongozi, sikuwa mjumbe wa bodi wala mwenyekiti wa timu hii kama nilivyo sasa,” amesema.

Ameongeza “lakini baada ya kuingia kwenye uongozi hili suala lilipelekwa kwenye bodi ya klabu na wajumbe tumelifuatilia na kubaini kuwa limeuzwa kwa kufuata utaratibu.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad