Nabii mkuu wa kanisa la Ngurumo ya upako ambaye pia ni balozi wa amani Dkt. Geordavie Kasambale amekabithi hundi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya ukarabati na kuwasaidia wajasiriamali wenye mitaji midogo katika soko la Samunge lililopo kata ya mjini kati mkoani Arusha.
Akikabithi hundi hiyo leo jijini Arusha katika soko la Samunge ,Nabii Mkuu amesema kuwa amewiwa kufanya hivyo baada ya kupata barua aliyoandikiwa ya kuhitaji msaada kwa ajili ya kukarabati na kusaidia wajasiriamali wenye mitaji midogo katika soko hilo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Amesema kuwa, kiasi cha shilingi milioni 80 watagawiwa mtaji wajasiriamali wenye mitaji midogo na huku kiasi kilichobaki cha milioni 20 kikitumika kwa ajili ya kukaratabati soko hilo.
“Mimi huu msaada ninatoa sitafuti waumini sipo hapa kumbadilisha mtu dini nipo hapa kuwasaidia wananchi katika kuondokana na matatizo mbalimbali na asanteni sana kwa mabango na picha haya ni mahaba makubwa sana na asanteni kwa heshima yenu ya kunipa kuwa mlezi wa soko ila mniwie radhi tutakuwa tunashirikiana popote mnapohitaji msaada ila swala la kuwa mlezi sitaweza maana nina majukumu mengi sana,” amesema Nabii.
Amesema kuwa, kinachomsukuma kusaidia jamii ni Mungu kwani awali alipoitwa kutumikia Mungu alipewa maono ya kueneza injili ya kinabii na aliifanya lakini Kwa Sasa Mungu alimwambia afanye injili kwa matendo na ndio maana ameanza kueneza matendo kama Moja ya kauli mbiu yake inavyosema maneno machache kazi kubwa zaidi.
Aidha amewataka Viongozi wa dini kutochukua sadaka tu wakati umefika wa kuanza kurudisha kile wanachokipata kwa wananchi ,ni wakati sasa kurejesha fadhila kwa jamii wawasaidie maana watu wanateseka ,hivyo ni vyema wakajitoa na kujitahidi kuwasaidia wenye uhitaji.
“Msaada huu nilioutoa ni baada ya kupokea barua yenu ya kuomba msaada na nimekuja kuwaunga mkono na kila mmoja anapaswa kutambua kuwa tunaposaidia jamii tutakuwa tumemsaidia pia Rais Samia Suluhu Hassan katika swala la maendeleo, unajua serikali inasaidia wananchi wake lakini haiwezi kuwafikia wote hivyo ni vyema watu kama sisi tujifunze kujitoa na kuwasaidia wenye uhitaji. “amesema.
Naye Mbunge wa Arusha mjini,Mrisho Gambo amesema kuwa,kazi ya viongozi wa serikali ni kuwaheshimu viongozi wote wa dini na kuwapa heshima yao pamoja na kuheshimu kipawa walichopatiwa ,aliongeza kuwa Mungu tunaemuabudu ni mmoja sema majina tu ndio yanatofautiana hivyo ni vyema Kila mmoja akaheshimu imani ya mwenzake.
Gambo amesema kuwa, mnamo mwaka 2019 soko liliungua kwa moto na tangu lilipoungua walijisaidia wenyewe na wameendelea kuishi kwenye changamoto hiyo kwa muda mrefu bila kupata msaada wowote kutoka popote hivyo alimshukuru nabii Mkuu Kwa kuguswa na kuja kuwasaidia wafanya biashara hao.
“Hapa soko la Samunge tunakabiliwa na changamoto ya ukarabati wa soko kwani mvua ikinyesha matope na mvua ni ya kwao ,sambamba na usumbufu mkubwa wa mgambo wanaoupata sokoni hapa baba naomba utoeneno Kwa ajili ya hawa migambo ili waache,” amesema.
Amesema kuwa ,amewahi kutoa kiasi cha shilingi milioni 20 kama mtaji kwa wanawake wa soko hilo kwa ajili ya kuwasaidia wanawake kuondokana na changamoto mbalimbali.
lakini katika kuhakikisha anasaidia ukarabati wa soko hilo na kumuunga mkono Nabii mkuu ameaidi kutoa kiasi cha shilingi Milioni 10 .
Amefafanua kuwa,Rais Samia ameonyesha njia tayari na anaenda kujenga soko la kisasa kilombero na kwa mrombo pia .
Diwani wa kata ya Mjini kati, Abdulrasul Tojo amesema kuwa , wanaenda kuweka historia kwa kujenga hoja baraza la madiwani ili soko hili liwe chini ya nabii mkuu.
Aidha Diwani huyo walimwomba Nabii Georgdavie kuwa soko hili liwe chini yake kwani tangu lilipo ungua limekuwa katika hali ya mbaya hadi sasa hivi.
Akisoma risala kwa niaba Wafanyabishara wa soko la Samunge Katibu wa afya wa soko la Samunge Loveless Joakim amesema kuwa, soko la NMC lilianzishwa mwaka 2012 kwa lengo kusaidia wafanyabiashara wadogo ambapo alisema soko hilo lina zaidi ya wafanyabiashara 2,106.
Amesema kuwa, walipata changamoto kuunguliwa na soko hilo mwaka 2019 na baada ya hapo miundombinu mingi iliharibika na kupelekea kila mmoja kujijengea soko na mahitaji mengine huku bado wakiendelea na changamoto hiyo.