NBC Yakabithi Zawadi Kwa Mchezaji Bora na Kocha Bora wa Mwezi Ligi Kuu


Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara (NBC Premiere League) jana ilikabidhi zawadi ya pesa na tuzo kwa mchezaji bora wa ligi hiyo wa mwezi Desemba, Clatous Chama pamoja na kocha bora wa mwezi huo, Juma Mgunda wote kutoka klabu Simba SC.

Makabidhiano ya zawadi hizo yalifanyika muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo baina ya Simba SC dhidi ya Mbeya City FC uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, mchezo ambao ulimalizika kwa timu ya Wekundu wa Msimbazi Simba kuibuka na ushindi wa goli 3-2.

Katika tukio la makabidhiano ya zawadi hizo, ilishuhudiwa Mkurugenzi wa Udhibiti Majanga Benki ya NBC, Godliving Maro akikabidhi mfano wa hundi ya pesa yenye thamani ya Sh1 milioni kwa kiungo wa Simba, Clatous Chama pamoja na tuzo sambamba na kisimbuzi cha Azam huku pia Kocha Mgunda kutoka timu hiyo akipatiwa mfano wa hundi yenye kiasi kama hicho cha pesa, tuzo na kingamuzi cha Azam.

“Kimsingi ni kwamba sisi kama wadhamini wa ligi hii tunaendelea kujivunia sana kuona ligi yenye ushindani na viwango bora vya kiuchezaji vinavyoendelea kuonekana kwenye ligi hii. Ndiyo maana utaona kwamba pamoja na ligi kuwa na wachezaji wengi wa kigeni bado wachezaji wazawa wanapambana na kufanya vizuri na wanachukua tuzo hizi. Huu ni uthibitisho kwamba vilabu vyote kwasasa vinaweza kuhudumia vyema wachezaji wake kiasi cha kuweza kutoa ushindani unaotakiwa,’’ alisema.

By Mwandishi Wetu
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad