Necta Yatoa Ufafanuzi Matokeo ya Mvulana Shule ya Wasichana



Dar es Salaam. Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limesema jinsia ya kiume inayoonekana kwenye orodha ya matokeo ya kidato cha nne katika shule ya wasichana ya Musabe ni msichana.

Kauli hiyo ya Necta inakuja ikiwa ni siku moja imepita tangu itangaze matokeo ya mitihani ya kidato cha nne uliofanyika Novemba 14 hadi Desemba 1, 2022.

Katika matokeo hayo, orodha ya majina ya wanafunzi wa shule ya Wasichana Musabe ya jijini Mwanza kuna jina la mwanafunzi wa kiume, hali iliyoibua mjadala mkali maeneo mbalimbali ikiwemo mitandaoni.

Watu wamekuwa wakihoji imewezekanaje shule yenye wasichana pekee tena ya kulala awepo mvulana aliyefanya mtihani?


Kutokana na hilo, Mwananchi Digital, leo Jumatatu Januari 30,2023 limemtafuta Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athumani Amasi kutaka kujua suala hilo ambapo amesema hayo ni matatizo ya usajili na huyo si mvulana bali ni msichana.

Athumani amesisitiza,“hayo ni matatizo ya usajili jina na jinsia zitabadilishwa.”

Jinsia hiyo iliyoibua mjadala ni miongoni mwa wanafunzi 138 katika shule hiyo ambayo wanafunzi wote 138 wamepata daraja la kwanza.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad