Nyaraka Zaidi Za Siri Zapatikana Kwenye Nyumba Ya Rais Wa Marekani Joe Biden



Wachunguzi wa Idara ya Haki ya Marekani (DoJ) wamepata hati sita zaidi za siri wakati wa upekuzi wa saa 13 katika nyumba ya Rais Joe Biden huko Delaware, wakili wa Biden anasema.


Baadhi ya stakabadhi zilizonaswa katika eneo la Wilmington siku ya Ijumaa zilikuwa za wakati akiwa seneta na nyingine za kipindi akiwa makamu wa rais chini ya Barack Obama. Wakili Bob Bauer alisema “noti zilizoandikwa kibinafsi” na “vitu vingine” pia zilichukuliwa.


Bwana Biden na mkewe hawakuwepo. Rais alitoa nafasi “nyumbani mwake ili kuruhusu DoJ kufanya upekuzi katika majengo yote kwa rekodi zinazowezekana za makamu wa rais na vingine vinavyoweza kuainishwa”, Bw Bauer alisema katika taarifa yake Jumamosi.




Mapema mwezi huu mawakili wa Bw Biden walisema kundi la kwanza la hati za siri lilipatikana tarehe 2 Novemba katika Kituo cha Penn Biden, taasisi ambayo rais aliianzisha Washington DC.


Kundi la pili la rekodi lilipatikana tarehe 20 Desemba katika gereji nyumbani kwake Wilmington, wakati hati nyingine ilipatikana katika nafasi ya kuhifadhi kwenye nyumba hiyo mnamo Januari 12, mawakili wake walisema.


Baada ya kupata hati hizo, rais alisema timu yake ilizikabidhi mara moja kwa Hifadhi ya Kitaifa na Idara ya Haki. Haijabainika kwa nini Bw Biden alikuwa amezihifadhi. Chini ya Sheria ya nyaraka za Rais, rekodi za Ikulu ya White House zinapaswa kwenda kwa Kumbukumbu za Kitaifa, ambapo zinaweza kuhifadhiwa kwa usalama.


Wakili maalum, Robert Hur, ameteuliwa kuongoza uchunguzi wa jinsi nyaraka hizo nyeti zilivyoshughulikiwa. Utafutaji wa muda mrefu na ugunduzi uliofuata wa hati zaidi ni maumivu ya kisiasa kwa rais, anapojiandaa kutangaza ikiwa atagombea muhula wa pili mnamo 2024.


Bw Biden na mkewe, Jill siku za wikendi hukaa katika mji wa pwani wa Rehoboth Beach huko Delaware, ambapo wanamiliki nyumba nyingine.


Ilikaguliwa mapema mwezi huu na hakuna hati zilizopatikana, mawakili wake walisema, kwa mujibu wa New York Times.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad