Polisi Adaiwa Kumvunja Raia Miguu Kwa Tuhuma za Kuwa na Uhusiano na Mkewe



Mkazi wa Mtaa wa Mlimani 'A' Wilayani Ilemela, Mohammed Khatibu (29) anadaiwa kuvunjwa miguu na Mkuu wa Kituo kidogo cha Polisi Kiseke aliyekuwa akimtuhumu kuwa na Uhusiano na Mke wake

Inaelezwa Khatibu alikamatwa Januari 3, 2023 na Askari huyo kwa kushirikiana na rafiki yake, wakitumia Gari binafsi bila kumweleza kosa lake. Walisema wanampeleka Kituo cha Polisi Kirumba na badala yake alipelekwa Kiseke ambapo alipigwa

Mama wa Khatibu amesema baada ya kumkosa Mwanaye Kituo cha Kirumba, walipata fununu yupo Kituo cha Kiseke lakini nako waliambiwa hayupo. Hata hivyo alizunguka nyuma ya Mahabusu na kuita Jina la Mwanaye, ambapo aliitikia akiwa Mahabusu humo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad